Tovuti Hii Imejikita Katika Dini Ya Kiislamu Tu. Lengo Kuu La Tovuti Ni Kueneza Uislamu Safi Aliokuwa Nao Mtume Swalla Allahu ‘Alayhi Wasallam, Maswahaba Zake Na Wale Waliowafuata Wao Kwa Wema, Ambao Wote Wanatambulika Kwa Jina La “السلف الصالح” Wema Waliotangulia. Kutokana Na Hilo Ndio Limepatikana Jina La Tovuti Hii salafussaalih.net.
Tovuti Hii Imeanzishwa Mwaka 1439 Hijiria Sawa Na Mwaka 2018 Miladia. Inaendeshwa Na Wanafunzi Vijana Wenye Kujifunza, Kufanyia Kazi Na Kuyasambaza Yale Wanayojifunza Au Kufundishwa Yawafikie Wengine Hasa Jamii Ya Wazungumzaji Wa Kiswahili Inayopatikana Ukanda Wa Afrika Mashariki Na Sehemu Nyingine Za Ulimwengu.
Tovuti Hii Inaendeshwa Kwa Hali Na Mali Za Kujitolea Sadaka Wasimamizi Wenyewe, Haifadhiliwi Na Serikali, Na Wala Haifungamani Na Chama Chochote Cha Kisiasa Au Makundi Yaliochupa Mipaka Kama Khawaarij N.k Yasiofuata Qur-aan Na Sunnah Kwa Ufahamu Wa Wema Waliotangulia.
Katika Kuchunga Amana Hii Adhimu Tumechagua Kuweka Maudhui Za Uandishi, Picha, Video Na Sauti Ambazo Zimetolewa Na Walimu, Maustadh, Masheikh Au Wanavyuoni Ambao Wamesalimika Manhaj Yao Wakati Wa Kuhudhurisha Maudhui Hizo.