Kufikiwa Na Ramadhani Ni Neema Kubwa
بلوغ رمضان نعمة كبيرة
قال العلَّامة ابن عثيمين رحمه الله :
Amesema Al Allaama Ibnu Uthaymeen ALLAH amrehemu:
“إخواني: بلوغ رمضان نعمة كبيرة على من بلغه وقام بحقِّه;
Ndugu Zangu: Kufikiwa Na Ramadhani Ni Neema Kubwa Kwa Yule Ambaye Imemfikia Na Akasimama Kwa Haki Zake,
بالرُّجوع إلى ربِّه، من معصيته إلى طاعته،
Kwa kurejea kwa Mola wake kutoka katika kumuasi yeye kwenda katika kumtii yeye,
ومن الغفلة عنه إلى ذكره،
Na kutoka katika kughafilika nae mpaka kufikia kumtaja yeye,
ومن البعد عنه إلى الإنابة إليه.”
Na kutoka katika kuwa mbali nae mpaka kufikia kurejea kwake.
(مجالس شهر رمضان: ص:١٩)
NENO LA ZIADA
Ndugu Zangu Waislamu, Moja Katika Neema Iliyokuwa Kubwa Sana Ambayo Mtu Apaswa Aikariri kwa Kumshukuru ALLAH ni Kumfikisha Yeye Katika Mwezi Wa Ramadhaani Akiwa na Afya na Siha Kadhalika Akaweza Kuyatimiza Yote Yanayompasa Kwa Kurejea Kwa Mola wake Mlezi Kutokana na Makosa Ambayo Aliyafanya Kwenye Miezi Iliyopita.
Vilevile Kuongeza Juhudi ya Kumtii ALLAH kwa Kutekeleza Yote Yanayomlazimu na Kuacha Yote Yanayomkasirisha ALLAH .
Katika Ibada Zilizokuwa Kubwa Mtu Kudumu Nazo Katika Mwezi Wa Ramadhaani Ni Pamoja Na:
-Kukithirisha Kusoma Qur-an.
-Kukithirisha Kumtaja ALLAH.
-Kujilazimisha Kuzihifadhi Sala za Jamaa.
-Kujihimiza Kuzihifadhi Sala Za Sunnah (Hususan Qabliyah na Baadiyyah)
-Kukaa Vikao Vya Kujifunza Elimu ya Kumjua ALLAH.
-Kukithirisha Kutoa Sadaqa.
-Kuunga Ukoo.
-Kuwakirimu Mayatima
-Na Mengine Mengi Katika Ibada.
Imeandikwa Na: Ustaadh Abu Luqmaan Omar Bin Othmaan
Imehaririwa Na: https://salafussaalih.net/
Imechapishwa Tarehe: 13 Shaabani 1443H ~ 16-03-2022M