Ni Ipi Hukmu Ya Sijda Ya Kushukuru Kwa Wachezaji Viwanjani?

قال الشيخ الصالح الفوزان حفظه الله

Amesema sheykh Swaleh Alfawzaan Allah amuhifadhi

الجواب
Jawabu

 

الكرة ولعب الكرة ما هو بنعمة ، وسجود الشكر إنما يكون عند تجدد نعمة ،

Mpira na kucheza mpira sio neema ,na hakika sijda ya shukrani inakuwa wakati wa kupatikana neema mpya,

 

فهو بدعة في هذا الموضع ،

Kwa hiyo ni UZUSHI katika sehemu hii

 

إيش حصلنا من الكرة هذه؟ وإيش المسلمون استفادوا منها؟

Kitu gani tumepata katika huu mpira? Na nini wamefaidika waislamu katika mpira?

 

إلا ضياع شبابهم ، ما استفادوا

Isipokua ni kupotea kwa watoto wao hawajapata faida ya chochote

 

بل هي ضرر على المسلمين.

Bali Mpira una madhara kwa Waislamu

 

من شرح فضيلته لمختصر زاد المعاد للشيخ محمد بن عبد الوهاب رحمه الله في يوم الأحد. 22/5/1430

 

NENO LA NYONGEZA:
Aliposema Sheykh juu ya madhara ya mpira kwa waislamu, ni kwa yale yanayopatikana ndani yake. Hasa hasa kwa vijana wa Kiislamu:

– Kutokuchunga Sala Zao.

– Namna ya uvaaji kwa wachezaji wa Mpira.

– Mashindano ya mpira ambayo yapo katika muundo KAMARI.

– Matangazo ya Biashara za HARAMU ndani yake.

– Kuumizana baina ya wachezaji uwanjani.

– Kupewa kipaombele zaidi mpira kuliko mambo ya msingi katika dini kwa Waislamu.

– Baya zaidi nalo ni Wanawake kuingizwa katika balaa hili.

 

Unamkuta anaesujudu baada ya kufunga goli hata kuswali haswali.

Na Mengineyo Mengi.

 

Imeandikwa Na: Ustaadh Abuu Luqmaan Omar.

Imehaririwa Na: salafussaalih.net

Imechapishwa Tarehe: 19 Shaabani 1443H ~ 22-03-2022M