Hukmu Ya Kusherehekea Usiku Wa Nusu Ya Shaaban
قال علماء اللجنة الدائمة للإفتاء:
Wamesema Wanawachuoni Wa Kamati Ya Kudumu Ya Fatwa
“لا يجوز الاحتفال بمناسبة ليلة القدر ولا غيرها من الليالي ولا الاحتفال لإحياء المناسبات؛ كليلة النصف من شعبان، وليلة المعراج، ويوم المولد النبوي؛
“Haifai kusherehekea Kwa Kunasibisha Na Usiku Wa Makadirio (Laylatul Qadri) Wala Mwengine Wowote Katika Usiku, Wala Kusherehekea Kwa Kuhuwisha Yale Yanayo Nasibiyana, Kama Usiku Wa Nusu Ya Shaabani, Na Usiku Wa Miiraji, Na Siku Aliyozaliwa Mtume Sala Na Salamu Ziwe Juu Yake.
لأن هذا من البدع المحدثة التي لم ترد عن النبي صلى الله عليه وسلم ولا عن أصحابه،
Kwa Sababu Huu Ni Miongoni Mwa Uzushi Uliozushwa Ambao Haujaja Kutoka Kwa Mtume Sala Na Salamu Ziwe Juu Yake.
وقد قال صلى الله عليه وسلم: (من عمل عملا ليس عليه أمرنا فهو رد)، ولا يجوز الإعانة على إقامة هذه الاحتفالات بالمال ولا بالهدايا ولا توزيع أكواب الشاي،
Na Kwa Hakika Amesema Mtume Wa Allah Sala Na Salamu Ziwe Juu Yake Amesema (Yoyote Atakaye Fanya Kitendo Chochote Hakuna Juu Yake Amri Yetu Hichi Ni Chenye Kurejeshwa).
Na Wala Haifai Kusaidia Kusimamisha Sherehe Hizi Kwa Mali Na Zawadi Wala Kugawa Vikombe Vya Chai
ولا يجوز إلقاء الخطب والمحاضرات فيها؛ لأن هذا من إقراراها والتشجيع عليها، بل يجب إنكارها وعدم حضورها.”
Wala Haifai Kutoa Khutba Na Mihadhara Inayohusiana Na Usiku Huo Kwa Sababu Hilo Ni Katika Kuithibitisha Na Kushajihisha Hayo, Bali Inawajibika Kuipinga Na Kutohudhuria.“
من “فتاوى اللجنة الدائمة ”
(2/257 – 258)
NENO LA NYONGEZA
Usiku Wa Nusu Ya Shaabani Ni Sawa Na Usiku Mwengine Katika Mwaka. Haujahusishwa Kwa Chochote Katika Ibada.
– SI Kwa Kisimamo Chochote Kile Cha Swala Kilicho Maalumu.
– SI Kwa Kisomo Chochote Kile Maalumu Cha Qur-aan.
– SI Kwa Aina Yoyote Ile Ya Uradi Wala Adhkar Maalum.
– SI Kwa Funga Yoyote Ile Katika Mchana Wake
Na Katika makosa Kuitakidi Kuwa Huo Ndio Usiku Wa Kugaiwa Rizki (Qasmatu Rizki), Wakati Hilo Lipo Katika Laylatul Qadri.
KUITAKIDI KINYUME CHAKE NI ITIQADI ISIYO SAHIHI
Imeandikwa Na: Ustaadh Abuu Luqmaan Omar
Imehaririwa Na: salafussaalih.net
Imechapishwa Tarehe: 14 Shaabani 1443H ~ 17-03-2022M