2. Faida Kunako Hadiyth Za Mtume صلى الله عليه وسلم

 

قال رسول الله صلى الله عليه وسلم:-

Amesema Mtume wa Allaah swalaah na salamu ziwe juu yake:-

ثلاثةٌ كلُّهم ضامنٌ علَى اللَّهِ إن عاشَ رزقَ وَكُفيَ وإن ماتَ أدخلَهُ اللَّهُ الجنَّةَ،

(Watu wa aina) tatu wote ni wenye kuhifadhiwa na kuchungwa na Allaah na kama ataishi (mmoja wao) atapewa riziki na atatoshelezwa na kama atakufa atamwingiza peponi,

مَن دخلَ بيتَهُ فسلَّمَ فَهوَ ضامنٌ على اللَّهِ،

Yeyote atakayeingia nyumbani kwake na akatoa salamu basi (mtu) huyo atahifadhiwa na Allaah na kuchungwa,

ومَن خرجَ إلى المسجِدِ فَهوَ ضامنٌ علَى اللَّهِ،

Na yeyote mwenye kutoka na kuelekea msikitini basi (mtu) huyo atahifadhiwa na Allaah na kuchungwa,

 ومَن خرجَ في سبيلِ اللَّهِ فَهوَ ضامنٌ على اللَّهِ.

Na yeyote mwenye kutoka kuelekea katika jihadi basi huyo atahifadhiwa na Allaah na kuchungwa.

صححه العلامة محمد ناصر الدين الألباني في [صحيح الترغيب (٣٢١)].

Imesahihishwa na mwanachuoni Muhammad Naasird Diyn Al-Albaaniy Allaah amrehemu katika [Swahiyhit Targhiyb (321)].

 

Imeandaliwa Na: http://www.salafussaalih.net

Imechapishwa Tarehe: 14 Jumaadal Aakhirah 1443H ~ 17-01-2022M