1. Faida Kunako Hadiyth Za Mtume صلى الله عليه وسلم
عَنْ أَبِيْ أُمَامَةَ،عَنْ رَسُولِ اللهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ؛قَالَ:-
Imepokewa kutoka kwa Abiy Umaamah, (ambaye amepokea) kutoka kwa Mtume wa Allaah swalaah na salamu ziwe juu yake; amesema:-
[إِنَّ صَاحِبَ الشِّمَالِ لِيَرْفَعُ الْقَلَمَ سِتَّ سَاعَاتٍ عَنِ الْعَبْدِ الْمُسْلِمِ الْمُخْطِئِ أَوِ الْمُسِيءِ،
فَإِنْ نَدِمَ وَاسْتَغْفَرَ اللهَ مِنْهَا أَلْقَاهَا،وَإِلَّا كُتِبَتْ وَاحِدَةً].
Hakika (Malaika) wa upande wa kushoto huinyanyua kalamu masaa sita kwa mja muislamu mkosa au mtenda ovu, basi akijuta na kutubia kwa Allaah anaiweka (kalamu wala hamuandikii), na bila hivyo huandikiwa (kosa) moja.
هذا الحديث حسنه الألباني رحمه الله في [صحيح الجامع الصغير (٢٠٥٧)]،
وقال رحمه الله في [السلسلة الصحيحة (٢١٠\٣)].
Hadithi hii ameihasanisha Sheikh Albaaniy Allaah amrehemu katika [Swahiyhil Jaami’is Swaghiyr, nambari (2057)] na amesema Sheikh Albaaniy Allaah amrehemu katika [As-silsilatis Swahiyha (3/210)].
Imeandaliwa Na: http://www.salafussaalih.net
Imechapishwa Tarehe: 14 Jumaadal Aakhirah 1443H ~ 17-01-2022M