1. Neema Ya Amani
الأمن من أعظم النعم التي لا يستغني عنها الفرد ولا المجتمع.
Amani Ni Miongoni Mwa Neema Kubwa Zaidi Ambayo Hawezi Kutosheka Nayo Mtu Mmoja Mmoja Wala Jamii Kiujumla. (Kila Mmoja Ni Mwenye Kuhitajia Hio Amani).
Na Allaah ﷻ Juu Ya Waja Wake Ana Neema Kubwa! Na Katika Miongoni Mwa Neema Zake Hizo, Ambazo Zipo Mbele Zaidi Kwa Waja Wake Ni Neema Ya AMANI.
Haiwezi Kusimama Dini Wala Imani Wala Mambo Ya Kidunia Wala Maisha Ispokuwa Katika Hali Yakupatikana AMANI. Kila Mmoja Wetu Na Jamii Kiujumla Wanahitajia AMANI.
Bila Ya AMANI Hakuwezekani Kupatikana Maisha Mazuri Na Wala Maendeleo Katika Jamii Wala Kufanya Ibada Yoyote Ile Kwa Utulivu.
Wameghafilika Nayo Hio Neema Ya AMANI Wengi Katika Watu, Wala Hawaishukuru Neema Hio Ya AMANI Ispokuwa Watu Wachache Kabisa Katika Jamii.
Katika Mambo Yanayojuulisha Ubora Wa AMANI Nakuwa Ni Neema Kubwa Hio AMANI Ni Ile Kauli Yake Allaah ﷻ Aliposema Akimzungumzia Nabii Ibraahiim عليه السلام.
[وَإِذْ قَالَ إِبْرَاهِيمُ رَبِّ اجْعَلْ هَذَا بَلَدًا آمِنًا وَارْزُقْ أَهْلَهُ مِنَ الثَّمَرَاتِ …] [ البقرة:126].
“Na Kumbuka Alipo Sema Ibrahim: Ee Mola Wangu Mlezi! Ufanye Huu Uwe Mji Wa Amani, Na Uwaruzuku Watu Wake Matunda…..” [Surat al-Baqarah:126]
Akaanza Nabii Ibraahiim عليه السلام Kwa Kuomba Neema Ya Amani Kwanza Kabla Ya Kuomba Rizki, Itakapotulizana (Ikapatikana) Amani Ni Sababu Ya Kupatikana Rizki Na Kama Hakuna Amani Ni Ngumu Kupatikana Rizki.
وجاءَ فِي التفسيرِ الكبيرِ لِلرَّازِيِّ:
وَالابْتِدَاءُ بطلبِ نعمةِ الأمنِ فِي هذا الدعاءِ يدُلُّ على أنه أعظمُ أنواعِ النعمِ والخيراتِ، وأنه لا يَتِمُّ شيءٌ من مصالحِ الدينِ والدُّنْيَا إلا بهِ.
Na Imekuja Katika Tafsirul Kabiir Lirraaziy:
“Na Kuanza (Kwake Nabii Ibraahiim عليه السلام) Kuomba Neema Ya Amani Katika Dua Hii Inajuulisha Juu Ya Kuwa Hakika Hio Amani Ni Katika Aina Kubwa Zaidi Katika Neema (Nyingi) Na Kheri (Nyingi), Na Kuwa Hakika Hakuwezi Kutimia Kitu Chochote Kile Katika Maslahi Ya Dini Wala Dunia Ispokuwa Kwa kupatikana Kwake Hio (Amani).”
EWE NDUGU YANGU MUISLAMU USISHIRIKI KATIKA KUVUNJA AMANI YA NCHI YAKO KWA NAMNA YOYOTE ILE!!!
Itaendelea In Shaa Allah….
Mwandishi: Ustadh Abul Abbaas Anuari Ismail Ali Al-Zinjibaary Asshaafi’y, Allaah Amuhifadhi.
Mchapishaji: salafussaalih.net
Tarehe: 15 Rabiu al-Thaaniy 1447H